Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) imetoa mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Mei, 2025
kwa wadau wa Utalii kuhusiana na matumizi ya mfumo mpya wa Safari Portal V2
ulioboreshwa kutoka mfumo wa zamani wa Safari Portal.
Akifungua Mafunzo
hayo Kaimu Meneja wa Huduma za Utalii na masoko NCAA, Afisa Uhifadhi Mkuu Peter
Makutian ameeleza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wadau wote wa
Utalii kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa makusanyo ya mapato yatokanayo na
shughuli za Utalii ambao umeboreshwa ili kurahisisha utoaji huduma kwa wadau
wote wanaofanya kazi na NCAA.
"Tumeboresha
mfumo wetu wa makusanyo ya mapato ya Utalii na utaaanza kutumika kuanzia
tarehe 31/05/2025, kwa hiyo ni muhimu
wadau wetu wanaopata huduma kupitia mfumo huu wawe na uelewa ya maboresho
yaliyofanyika na kuwasaidia namna ya kuhamisha taarifa zao kwenye mfumo mpya
kabla ya tarehe ya kuanza mfumo huo," alilisitiza Makuatian.
Makutian ameongeza
kuwa sababu zilizopelekea kuboresha mfumo huo ni kuendana na mabadiliko ya
kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano sambamba na kuzingatia
mapendekezo ya Wadau wa utalii ambao ndio watumiaji wakuu wa mfumo huo.
Mafunzo hayo yameshirikisha
makundi mbalimbali katika mnyororo wa sekta ya utalii ikiwemo Waongoza watalii,
wamiliki wa kampuni za utalii, madereva wa utalii, wamiliki wa hoteli na wadau
wengine wanaohusika na sekta ya Utalii.
Wadau wa utalii
walioshiriki mafunzo hayo wametoa pongezi kwa uongozi wa NCAA kwa maboresho ya
mfumo huo ambao umerahisisha taratibu za malipo bila kutumia mda mrefu
wanapokuwa na shughuli za utalii na wageni ndani ya
hifadhi ya Ngorongoro.
Na. Kassim Nyaki- NCAA
0 Maoni