Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetumia fursa ya maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yanayofanyika jijini Dodoma kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 17 na kuhitimishwa leo Mei
20, 2025 katika Viwanja vya Chinangali Park Dodoma Mgeni rasmi akiwa ni Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, yamewakutanisha
wadau wa sekta ya nyuki kutoka Mikoa mbalimbali nchini kujadili maswala
yanayohusu sekta ya ufugaji nyuki katika uhifadhi na kuleta maendeleo endelevu
kwa jamii.
Katika maadhimisho hayo NCAA imepata fursa ya kutangaza
vivutio vyake vya utalii vikiwemo Bonde la kreta ya Ngorongoro lenye muonekano
wa pekee, wanyama mbalimbali ikowemo wa wanyama wakubwa watano “The big Five
“, Laitoli zinakopatikana Nyayo za
binadamu wa kale aliyeishi miaka milioni 3.7 iliyopita, Olduvai George eneo
lenye gunduzi za kihistoria ya akiolojia, Kreta ya Empakai iliyopambwa na ndege
aina ya Flamingo, Tambarare za Ndutu, Kreta ya Olmoti, Jabali la Nasera (Nasera
Rock”, Pango la Olkarien, Mchanga unaohama na vivutio vingine.
Akizungumza ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
kwenye maadhimisho hayo Afisa wa Uhifadhi- Utalii Joseph Mzaga amesema kwamba
maadhimisho haya yamewakutanisha na taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi
ambao wameza kuwaeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na NCAA kwenye Utalii,
Uhifadhi na maendeleo ya jamii.
“Maadhimisho haya yametupa fursa ya pekee ya kutangaza
vivutio vilivyopo ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa watu mbalimbali zikiwemo taasisi, watu binafsi na
makundi ya wanafunzi walioweza kukutembelea mahali hapa ambapo wameonesha
shauku kubwa ya kwenda kutembelea vivutio hivi,” alisema Joseph.
Katika kuelekea Mkutano wa 50 wa Kimataifa wa Shirikisho la
Umoja wa Vyama vya Wafugaji nyuki Duniani (Apimondia 2027) unaotarajiwa
kufanyika Tanzania, NCAA imejipanga kuonesha utajiri wa rasilimali za asili,
utalii wa kipekee na jitihada za uhifadhi
kupitia sekta ya nyuki na utalii.




0 Maoni