Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atupele
Mwambene akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru
kama Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, amefungua na kuendesha kikao kazi cha Kamati
Tendaji ya Mradi wa Green and Smart Cities Programme ambacho awali kilipokea
taarifa ya utekelezaji wa kazi zinazoendelea na zitatolewa maamuzi katika kikao
cha mwisho kinachotarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai, 2025.
Kwa upande wa Wadau wa Maendeleo Mwenyekiti mwenza Bw. Marc
Stalmans Mkuu wa ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa Tanzania na
Jumuiya ya Afrika Mashariki ameshiriki kikao hicho na kufurahia mipango na
makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Serikali ya Tanzania.
Aidha, kikao hicho kimepitisha masuala ya utekelezaji wa
Mradi wa Green and Smart Cities kwa kuidhinisha Serikali ya Denmark kujiunga na
Mradi huo ambapo Shilingi Bilioni 56 zinatarajiwa kupokelewa Serikalini,
kuidhinisha matumizi ya fedha za mkopo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa
(AFD) Shilingi Bilioni 189 na kuielekeza timu ya utekelezaji iweze kuongeza
kasi ya utekelezaji wa Mradi.
Kikao hiki cha Kamati Tendaji kimewahusisha Serikali ya
Tanzania kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya
Fedha, Wizara ya Maji, Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanga na Mwanza, Watendaji
kutoka Ofisi za Serikali zilizohudhuria, Wawakilishi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mashirikia na nchi
wanachama wa Umoja wa Ulaya.




0 Maoni