Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed
Mchengerwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria jukwaa la uchumi Arusha linalofanyika katika
Ukumbi wa IACC Arusha.
Kongamano hili limejumuisha zaidi ya wadau 1000 kutoka
maeneo mbalimbali duniani na kushirikisha mawaziri kadhaa wa sekta za tofauti.
Mwanamajumui wa Afrika Profesa Patrick Lumumba pia amealikwa kuwa miongoni mwa watoa mada.
Jukwaa hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul
Makonda ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa huo kupata ujuzi wa namna
ya kutumia fursa za uchumi zilizopo mkoani Arusha.
0 Maoni