Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof.
Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, ameeleza kuwa mkutano wa kwanza wa
kimataifa wa masuala ya habari, filamu na burudani (World Audiovisual &
Entertainment Summit-WAVES) unaoendelea katika jiji la Mumbai nchini India, umeifungulia
Tanzania fursa katika kuendeleza sekta za habari, filamu na burudani.
Mhe. Kabudi ameeleza fursa hizo leo Mei 3, 2025 mara baada
ya kufanya kikao cha pembezoni (side meeting) na Waziri wa Nchi, Wizara ya
Habari na Utangazaji wa India, Dkt. Roganathan Murugan, ambapo katika
mazungumzo, Mawaziri hao wamekubaliana kufufua upya kwa idhaa ya Kiswahili ya
Shirikia la Utangazaji la India la All India Radio kwa kushirkiana na Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) ili kukifanya Kiswahili kitangazwe na Radio hiyo
ya India na kukifanya kisikike tena katika Bara Hindi na sehemu zingine duniani
ambako All Radio India inasikika.
“Pmoja na hayo tumekubaliana tena kuanza kuwa na ushirikiano
wa kiufundi na All Radio India hasa katika mitambo mipya ya mipya utangazaji
radio ya kidigitali ya DRM 30+ ambapo India wenzetu wa India wapo mbali sana,
tumeweza kutembelea maonesho na tumeona jinsi gani India wamekwenda mbali sana
katika teknolojia ya utangazaji na urushaji wa matangazo,” ameeleza Prof.
Kabudi.
Waziri Kabudi ametaja maeneo mengine ya ushirikiano kuwa ni
katika eneo la utengenezaji wa filamu na kuangalia jinsi gani Tanzania na India
zinaweza kushirikiana katika kutengeneza filamu, maudhui ya filamu na
kuzisambaza filamu za Tanzania nchini India na za India kuendelea kununuliwa na
kutumiwa nchini Tanzania.
Aidha, amesema eneo linguine ambalo Tanzania inahitaji
kulitumia ili kuhakikisha soko lake la filamu linasambaa nchini India ni pamoja
na kuweka maneno ya tafsiri ya Kihindi na Gujirati kwenye filamu zinazotengenezwa
Tanzania ili ziweze kuuzika nchini India na pia kuangalia taasisi mpya ya India
inajihusisha na sanaa bunifu itakavyoweza kuchukua wanafunzi kutoka Tanzania.
“Chuo hicho ni kipya na kinasisitiza matumizi ya teknolojia
kuendana na mazingira ya nchini ambazo zinahitaji teknolojia hiyo”, amesisitiza
Mhe. Kabudi huku akionesha umuhimu kwa wasanii wa Tanzania kutumia fursa hiyo
ya mafunzo na tafiti katika kimarisha na kuboresha kazi za Sanaa.
Prof. Kabudi amemueleza Waziri wa Habari na Utangazaji wa
India, Dkt. Murugan juu ya uzuri wa Tanzania na kumueleza kuwa Tanzania
inawakaribisha watengeneza filamu kutoka India kutumia maeneo ya kimkakati
nchini kama Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro. Zanzibar na maeneo mengine kuyatumia
kurekodi filamu za kihindi na kuwaalika watu mashuhuri wa India wakiwemo
waigizaji na watengeneza filamu kuja kutembekea Tanzania na kuona maeneo
watakayoshirikiana na Bodi ya Filamu Tanznaia.
“Tumewakaribisha katika maonesho yetu ya filamu ya kila
mwaka kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) na Sinema Zetu, na wao
pia wametualika katika maonesho yao ya sinema ambayo mara nyingi yanafanyika
mwishoni mwa mwezi Novemba,” amesisitiza Mhe. Waziri Kabudi.
Mbali na kushiriki mkutano na kuoata fursa ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari na Utangazaji wa India, Mhe. Kabadi na ujumbe wake kutoka Tanzania walipata fursa ya kutembekea maonesho yanayoendana na mkutano huo pamoja na kwenda kujionea eneo maarufu Bollywood (Film City) ambalo hutumika kutengenza filamu nyingi za kihindi na kujifunza mambo mengi yatakayosaidia kwenye ujenzi yatakayosaidia wakati wa ujenzi wa Arts and Sports Arena.
0 Maoni