Wajumbe wa Mkutano
Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiburudika burudani ya mziki kutoka
Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre (TOT), kikiongozwa na Malkia wa
Mipasho na Mziki wa Taarab, Bi. Khadija Omar Abdallah Kopa, leo Ijumaa tarehe
30 Mei 2025, jijini Dodoma.
Mkutano Mkuu Maalum
wa CCM Taifa huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulianza jana Alhamis, tarehe 29 Mei
2025, na leo unaendelea katika siku yake ya pili, katika Ukumbi wa Mikutano wa
Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mojawapo ya agenda itakuwa ni kuzindua
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 - 2030.
0 Maoni