Kamishna wa Maadili Ofisi
ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji ( Mst.)
Sivangilwa S. Mwangesi amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi wa
taalumu yao kwa kutoa taarifa stahiki, zenye ulinganifu zitakazosaidia wananchi
kuwachagua viongozi waadilifu.
“Sote tunafahamu kuwa
mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani baada ya uchaguzi
tutapata viongozi watakaoliongoza taifa hili kwa kipindi cha miaka mitano, hivyo ni muhimu wananchi kuwachagua viongozi
waadilifu,” alisema Jaji Mst. Mwangesi.
Jaji Mst. Mwangesi
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na wahariri wa
vyombo vya habari wenye lengo la kuwaelewesha shughuli mbalimbali zinazofanywa
na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ameeleza kuwa juhudi
za wahariri katika ukuzaji wa maadili ya viongozi nchini zinaonekana wazi kwa
jinsi wanavyotumia kalamu zao kuelimisha, kuhabarisha, kuburudisha na kukosoa
jamii kuhusu dhana ya uadilifu kwa viongozi.
Ametoa raia kwa waandishi
wa habari kuendelea kutoa habari zinazohusu mienendo ya viongozi wa umma ili
wale wenye mienendo isiyofaa waweze kupata kujirekebisha ama wapate kuonywa na
mamlaka zinazowasimamia.
0 Maoni