Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi inayolenga kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Nishati.
Akiwa nchini humo, Dkt. Biteko anatarajiwa kukutana na
kuzungumza na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme
wa Morocco, Mhe. Leila Benali ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu
Sekta ya Nishati.
Mara baada ya kuwasili, Dkt. Biteko amepokelewa na Naibu
Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu nchini humo, Mhe. Mohamed
Ouhmed, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la
Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya
Nishati, Wakala wa nishati vijijini
(REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli
(TPDC).



0 Maoni