Katibu wa Jumuiya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Singida Bi. Naomi Daudi ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe.
Bi. Naomi ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la
TARURA kwenye maonesho ya maadhimisho ya Kitaifa ya Usalama na Afya mahali pa
kazi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mandewa mkoani Singida.
“Kilichonifurahisha hapa ni kwamba sasa tumeweza kuhamia
kwenye teknolojia ya mawe na matofari ya kuchoma ambapo inakuwa kwa gharama
ndogo.”
Amesema ubunifu huo wa watendaji wa TARURA itasaidia
serikali kupunguza gharama na miradi mingi kutekelezwa kwa wakati.
Hata hivyo ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya TARURA katika kipindi
chake na hivyo kuongeza ufanisi wa kazi na kusaidia kufungua barabara mpya
nyingi na kujengwa kwa madaraja na vivuko vingi nchini.
Naye , Fundi Sanifu Mwandamizi wa TARURA wilaya ya Singida Bw. Felix Mwaituka amesema kwamba matumizi ya teknolojia hiyo yameweza kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
0 Maoni