Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Neema Lugangira amependekeza suala la
udhibiti wa usalama wa chakula kuondolewa katika Shirika la Viwango nchini
(TBS) na kuhamishiwa katika Wizara ya Afya.
Mhe. Lugangira ametoa ushuri
huo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu,
ambapo amesema kwa sasa shirika la TBS limeshindwa kudhibiti suala la usalama
wa chakula.
“Kwa sasa Shirika la Viwango
TBS limeshindwa kudhibiti usalama wa chakula, tunapaswa kuacha kulifanya suala
la chakula kuwa la kibishara…hivyo basi napendekeza suala la udhibiti wa
usalama wa chakula lihamishiwe Wizara ya Afya,” amesema Mhe. Lugangira.
Amesema hali ya sasa ya
vyakula vinavyotoka ndani na nje vinavyouzwa sokoni hairidhishi, kwa maana ya usalama wa chakula (food safety).
“Hatuwezi kuendelea kufanya suala la usalama wa chakula kibiashara, suala la
usalama wa chakula ni suala linalohusu uhai na afya za Watanzania.”
Pamoja na mamo mengine, Mhe.
Lugangira ameitaka Serikali kutoa kauli Bungeni ya kuirejesha Taasisi ya Chakula
na Lishe (TFNC) kama ilivyoona umhimu wa kurejesha Shirika la Elimu Kibaha, kutokana
na umuhimu na uhitaji wa TFNC kwa Watanzania.
Pia, Mhe. Lungangira
amependekeza TFNC ihamishiwe kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ambaye kwa sasa ofisi
yake ndio inaratibu masuala ya lishe kwa sababu suala ya lishe ni suala
mtambuka.
0 Maoni