Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejidhatiti kuendelea kukuza na kuimarisha sanaa nchini ikiwa ni moja ya sekta rasmi ya kiuchumi.
Ametoa kauli hiyo leo
Jumapili (Aprili 13, 2025) katika Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio
Tanzania, linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha. Ambapo amesema fani ya
ushereheshaji ni uchumi.
Amesema kuwa kwa kutambua
umuhimu huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kaunzisha Mfuko wa
Utamaduni na Sanaa ambao unakopesha hadi shilingi Milioni 100 kwa wasanii
wakiwemo washereheshaji ili waweze kujiimarisha kimitaji na vitendea kazi.
“Pia kupitia maboresho ya
Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 yaliyofanyika mwaka 2022,
Serikali imeanzishwa tozo ya hakimiliki (copyright levy) ambapo asilimia 60 ya
makusanyo inakuja kwenu moja kwa moja na asilimia nyingine 10 inakuja kwenu
kupitia Mfuko.”
Katika hatua nyingine,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga Ukumbi wa
Kimataifa ya Sanaa na Michezo ‘Arts and Sports Arena’ kwa shilingi bilioni 300.
“Haya yote ni maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa
ameaigiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) kushirikiana chama cha Kisima cha Mafanikio katika kuandaa
miongozo, mafunzo ya kitaaluma, na mfumo wa urasimishaji wa washereheshaji
nchini.
“Baraza la Kiswahili la
Taifa (BAKITA) endeleeni kushirikiana na Kisima cha Mafanikio katika kukuza
matumizi sahihi ya Kiswahili kwenye majukwaa mbalimbali.”
Kadhalika Mheshimiwa
Majaliwa amesema Serikali inatambua kazi ya Chama cha Kisima cha Mafanikio.
“Hakika kazi yenu ni ya msingi, nyeti na yenye mchango mkubwa kwa Taifa.”
Kwa Upande wake, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amemshukuru Rais
Dkt. Samia kwa uongozi wake mahiri na kwa kutoa fursa kwa watanzania kukuza
vipaji vyao na kuendeleza stadi za kazi na taaluma katika tasnia mbalimbali
ikiwemo ya ushereheshaji na upangaji wa matukio.
“Hakika Mheshimiwa Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan amekuwa katika mstari wa mbele wa kulea vipaji vyote na
kuvipa nafasi kuweza kuonekana na kutenda kazi zao kama ilivyokwenu watu wa Kisima
cha Mafanikio.”
Kwa Upande wake Mwenyekiti
wa Chama hicho Ester Kimweri ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoomgozwa
na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia uzalendo nchini.
“Sisi wadau wa sekta hii
tunapenda kuonesha nia yetu ya dhati kuendelea kuunga mkono juhudi hizi kwa
vitendo kwa kuuelimisha, kuuhamasisha, kuburudisha na kufundisha na sisi
tutaendelea kuheshimu sheria, kulinda rasilimali, mali za umma, kushiriki
shughuli za maendeleo ya jamii.”
0 Maoni