Rais wa
Zambia Hakainde Hichilema amewaonya mawaziri wanaolala wakati mikutano, jambo
ambalo amelihusisha na mienendo yao ya maisha ya kuponda raha bila kujidhibiti.
Hakufafanua
zaidi kauli yake hiyo, lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaeleza kuwa
alikuwa analenga tabia mawaziri za unywaji pombe kupindukia na sherehe za usiku
wa manane.
Rais Hichiema
ameonya kwamba tabia kama hizo zinaweza kuchangia kuvuja kwa siri za taifa na kupelekea
kuchelewesha utoaji huduma za jamii.
0 Maoni