Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi Aprili, zitakazotumika kuanzia leo, Jumatano, tarehe 02 Aprili 2025 saa 6:01 usiku.
Kwa mwezi
huu, gharama za uagizaji mafuta (premiums) zimepungua kwa wastani wa asilimia 6.08
kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.09 kwa mafuta dizeli na kuongezeka kwa
asilimia 1.11 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam, huku bandari
ya Tanga kukiwa hakuna mabadiliko, na kwa bandari ya Mtwara zimepungua kwa
wastani wa asilimia 4.00 kwa mafuta ya petroli na dizeli.
Katika bei
kikomo kwa mwezi Aprili 2025, bei za mafuta katika soko la dunia zimepungua kwa
asilimia 6.92 ya kwa mafuta ya petroli, asilimia 6.57 kwa mafuta ya dizeli na
asilimia 7.82 kwa mafuta ya taa mtawalia. Bei zinazozingatiwa za mafuta
yaliyosafishwa (FOB) ni za soko la Uarabuni.
Taarifa ya
EWURA imesema kwa bei za mwezi Aprili 2025, wastani wa gharama za kubadilisha
fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umeongezeka kwa asilimia 1.91.
EWURA imesema
inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja
kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa tu. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka AGIZO hili.
0 Maoni