Maandamano yakumpinga Mnangagwa yasitisha shughuli zote

 

Maandanamo ya kitaifa yakumshinikiza ajiuzulu Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa yamepelekea kusitisha shughuli zote  kufungwa kutokana na raia kuamua kubakia nyumbani badala ya kuingia mitaa huku kukiwa na ulinzi mkali.

Idadi ndogo ya waandamanaji walijitokeza katika maandamano hayo ambayo yanaongozwa na mavetenari wa vita ambao wanamtuhumu Mnangagwa kwa rushwa na kutaka kung’ang’ania madarakani.

Kutokana na kujitokeza kwa idadi ndogo ya waandamanaji Zimbabwe, kiongozi wa maandamano hayo Blessed Geza kupitia akaunti yake ya mtandao wa X amewataka wananchi wa Zimbabwe kuacha uoga.

Mnangagwa aliingia madarakani mwaka 2017 kufuatia mapinduzi dhidi ya kiongozi aliongoza muda mrefu nchi hiyo hayati Robert Mugabe, na kwa sasa anahudumu kwa muhula wake wa pili wa na wa mwisho wa urais.

Chapisha Maoni

0 Maoni