Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amekabidhi
kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia
Suhulu Hassan, zawadi za mkono wa Eid kwenye vituo vya kulea watoto wenye
mahitaji maalum.
Mhe. Senyamule amekabidhi zawadi hizo zilizotolewa na Mhe.
Rais kwa walezi na viongozi wa vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman
‘Orphanage Center ‘ vilivyopo Jijini Dodoma Machi 30,2025.
“Kwa niaba ya Serikali, niendelee kuwashukuru na kuwapongeza
walezi wote mnaolea watoto kwenye vituo hivi, Mungu awabariki kwa upendo
mnaouonesha kwa watoto hawa,” Mhe.Senyamule.
Naye Kiongozi wa Kijiji cha Matumaini Padri Vicent Boselli
amesema kwa zaidi ya miaka 20 kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto wenye
maambukizi ya VVU na kuwapa matumaini ya upendo na kuishukuru Serikali kwa
kuwakumbuka kwenye kipindi hiki cha Sikukuu.
Kwa Upande wao Shadrack Hassan na Hazla Ramadhan ambao ni
miongoni mwa watoto wenye mahitaji wanaolelewa katika vituo hivyo wamemshukuru
Mhe. Rais pamoja na Uongozi wa Mkoa kwa zawadi hizo.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na mchele, mbuzi, katoni za juisi, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage na mahitaji mengine muhimu.


0 Maoni