Mgeni rasmi
katika sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango.
Sherehe hizo
zilizoongozwa na kauli mbiu: “ Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025
kwa Amani na Utulivu” zimehudhuriwa na viongozi
mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa.
Viongozi
wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa
Zungu, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe.
Abubakar Kunenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania Bara
na Zanzibar.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiongea jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete leo Aprili 2, 2025 Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya Shirika la Elimu ameshiriki katika sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasha moto Mwenge wa Uhuru wakati akizindua mbio za Mwenge huo leo Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya Shirika la Elimu.
0 Maoni