Waziri wa Maji Mh. Jumaa
Aweso amesema Rais Dkt. Samia S. Hassan ameelekeza utekelezaji wa miradi ya
maji yenye thamani ya Bilioni 45 kutatua changamoto ya Maji Jijini Dodoma
wakati ikisubiriwa utekelezaji wa Miradi ya kuleta maji kupitia Ziwa Victoria
na mradi wa Bwawa la Farkwa.
Waziri Aweso ameyasema hayo
leo wakati akishuhudia utiaji wa saini wa mkataba wa mradi wa kusambaza maji
kupitia visima vya maji vya Nzuguni A wenye thamani ya Tsh 5bn unaotarajiwa
kuwanufaisha watu 123,095.
“Mbunge wenu alileta maombi
kwa Mh. Rais Samia juu ya uchimbwaji wa visima virefu wakati wa mkutano wa Mh.
Rais pale Mpunguzi na sisi Wizara tukapata maelekezo ambayo tumeyafanyia kazi.”
Tunamshukuru Mh. Rais Samia
kwa kulivalia njuga suala la maji hapa Jijini Dodoma kwa kuelekeza utekelezaji
wa miradi ya maji ya zaidi Tsh 45bn ambayo itasaidia sana kupunguza tatizo la
mgao wa maji katika maeneo mbalimbali.
DUWASA inaendelea na
utekelezaji wa miradi mingine kama vile Nala (3.8bn), UDOM,(1.2bn), Mji wa
Serikali (35.6bn), n.k. Aidha wizara ya maji kwa kushirikiana na taasisi zake
(DUWASA na RUWASA) imeunda timu zinazo endelea na Utafiti wa Maji chini ya
Ardhi na Uchimbaji wa visima katika maeneo ya Mzakwe, Nzuguni, Kisasa,
Nkuhungu,Miganga, Zuzu, Msalato na Ihumwa.
Nipo hapa Jijini Dodoma na
kesho naanza ziara maalum kukagua utekelezaji wa miradi hii ili wananchi wa
Dodoma wapate maji ya uhakika” alisema Aweso.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amesema utekelezaji wa mradi wa usambazaji
kupitia Nzunguni utasaidia kupunguza adha ya mgao wa maji kwa wananchi wa
maeneo ya Nkuhungu,Miganga,Chidachi,Nzuguni, Kisasa-Bwawani,Mwangaza, Ipagala,
Ilazo, na Swaswa, Mpamaa na Njedengwa.
Akitoa taarifa yake
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Eng.
Aron Joseph amesema Mradi huu unalenga kuhudumia watu wapatao 123,095 katika
maeneo yaliyotajwa hapo juu.
Kukamilika kwa mradi huu
kutapelekea ongezeko la uzalishaji kutoka lita milioni 81 hadi 91 kwa siku sawa
na ongezeko la 30% kutoka chanzo cha Nzuguni.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akielezea utekelezaji wa mradi wa usambazaji kupitia Nzunguni.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akishuhudia utiaji wa saini wa mkataba wa mradi wa kusambaza maji kupitia visima vya maji vya Nzuguni A wenye thamani ya Tsh 5bn unaotarajiwa kuwanufaisha watu 123,095.
0 Maoni