Katika
kusherehekea Siku ya Afya Duniani leo Aprili 7, 2025, yenye kaulimbiu
"Mwanzo Mzuri wa Afya, Mustakabali wenye matumaini", Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan amechukua fursa hii kumtangaza na kuunga Mkono Kampeni ya Prof.
Mohamed Yakub Janabi kama mgombea kutoka Tanzania kwa nafasi ya Mkurugenzi wa
Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO - Afro).
“Ninaunga mkono maono yake ya kuwa na Afrika
yenye afya bora, imara, na yenye mafanikio, ambapo kila mtu atapata huduma bora
za afya, na ambapo mifumo ya afya itakuwa imara kukabiliana na changamoto za
baadaye,” alisema Mhe. Samia.
“Uzoefu wake
na utendaji kazi wake pamoja na mafanikio aliyoyapata yanajieleza yenyewe. Nina
imani kwamba, uongozi wake utaleta matokeo chanya ya afya na ustawi wa jumla
katika bara letu la Afrika.”
0 Maoni