Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi
amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu wa
Uingereza ambaye pia ni Muanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tony
Blair Institute for Global Change (TBI), Sir Tony Blair kwa ushirikiano wake
katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarish bandari, utalii , na kuwajengea uwezo
Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Serikalini (PDB).
Rais
Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waziri Mkuu Mstaafu huyo, alipomtembelea kwenye makaazi yake The
South Pavillion, Cotton Underwood Aylesbury, Uingereza jana tarehe 6 Aprili
2025.
Aidha, Rais
Dkt. Mwinyi amemhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani
na utulivu katika kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Naye Waziri
Mkuu Mstaafu Tony Blair amemuahidi Rais Dkt.Mwinyi kuendelea kushirikiana na
Zanzibar katika uchumi wa kidigitali,
utalii, uwekezaji kupitia Taasisi
yake ya TBI.
Mkutano huo
umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Dkt.Saada
Mkuya, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Mbelwa Kairuki, Balozi John
Ulanga, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
0 Maoni