Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri ya Sikukuu ya
Pasaka Wakristo nchini huku akiwaasa kujitoa kwa bidii katika utekelezaji wa
majukumu na kuendelea kuijenga jamii tunayoishi katika kweli:-
Kupita katika ukurasa wake wa Instagram, Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan ameandika:-
Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndugu zetu
Wakristo wanaadhimisha kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo.
Siku hii njema ikawe pia ya tafakari kwetu sote juu ya
upendo wetu kwa Muumba wetu na wenzetu; juu ya kujitoa kwa bidii na weledi
katika utekelezaji wa majukumu yetu popote pale tulipo; juu ya kuendelea
kujenga jamii inayoishi katika kweli; na juu ya haki ambazo daima huambatana na
wajibu kwetu sote.
Kwa pamoja, tuendelee kuliombea Taifa letu kheri, huku tukiishi na kutenda yale yanayoiwezesha nchi yetu kuendelea kubaki kuwa moja, imara, yenye amani na utulivu.

0 Maoni