Maandamano ya kumpinga Trump yatikisa Marekani

 

Maelfu ya waandamanaji wameandamana Jumamosi nchini Marekani kupinga hatua za hivi karibuni zinazochukuliwa na Rais Donald Trump.

Maandamano hayo ya “50501” yakiwa na maana waandamanaji 50, Majimbo 50, vuguvugu la 1, yanalengo la kuungana na maadhimisho ya miaka 250 ya Vita vya Ukombozi wa Marekani.

Nje ya Ikulu, kwa mawakala wa kampuni Tesla na kati kati ya miji mingi waandamanaji walipaza sauti zao kuonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya Rais Trump.

Wengi wa waandamanaji hao walitoa wito wa kurejeshwa kwa Kilmar Ábrego García, ambaye alitimuliwa Marekani na kupelekwa El Salvador.

Maandamano ya kisiasa yameanza kuwa ya kawaida Marekani, baada ya maandamano ya “Hands Off” ya mwezi Arili kuvutia makumi ya maelfu nchini Marekani.



Chapisha Maoni

0 Maoni