Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi
amewakaribisha Wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo
sekta ya Uchumi wa buluu, utalii,
usafiri wa baharini, uvuvi ,
nishati na miundombinu ya kidijitali.
Rais
Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Wakurugenzi wa
Taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na
Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London, Aprili
7, 2025.
Aidha, Rais
Dkt.Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea
kukua zaidi ya asilimia 7 kutokana na
uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.
Rais
Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa wawekezaji hao kuwekeza katika zao la Mwani,
ameeleza kuwa Zanzibar ndio mzalishaji namba moja wa zao hilo Afrika ambalo
soko lake linaendelea kukua zaidi.
0 Maoni