Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa
kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kuboresha miundombinu ambapo hivi
karibuni Taasisi ya UK Export Finance ya Uingereza imetoa dhamana kwa ajili ya
ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pemba pamoja na miundombinu ya
Barabara Unguja na Pemba.
Rais Dkt.
Mwinyi amesema hayo alipokutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Angela
Rayner jana tarehe 8 Aprili 2025, Jijini London.
Naye, Mhe.
Rayner ameeleza kuwa Serikali ya Uingereza imeweka kipaumbele cha kukuza
uchumi ambapo kupitia mahusiano na
mataifa rafiki itakuwa tayari kukuza biashara na uwekezaji Zanzibar.
Halikadhalika,
Tanzania na Uingereza zakubaliana kukuza zaidi ushirikiano katika biashara na
uwekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Mutual Prosperity
Partnership, makubaliano hayo yamefikiwa Aprili 8, 2025 wakati wa mazungumzo
baina ya Rais Dkt. Mwinyi na Naibu Waziri Mkuu huyo Jijini London.
0 Maoni