Rais Mstaafu wa Tanzania na
Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
amefanyamazungumzo na Rais wa Niger, Mhe. Jenerali Abdourahamane Tchiani katika
Ikulu ya Niamey April 16, 2025.
Katika mazungumzo hayo, Mhe.
Kikwete ambaye ni mwanadiplomasia nguli aliwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais
Samia kwa Jenerali Tchiani.
Aidha, katika mazungumzo
hayo, Mhe. Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia ambapo alielezea
kufurahishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Niger
na kusisitiza umuhimu wa kukuza na kuuimarisha zaidi katika nyanja za biashara,
uwekezaji na utalii.
Alisisitiza umuhimu wa nchi
za Afrika kubadilishana uzoefu na ujuzi ili utajili mkubwa wa maliasili uliopo
uweze kuvunwa na kuendelezwa kwa faida ya wananchi wa bara hilo.
0 Maoni