Mtanzania Steven Magombeka
Maarufu Kama Kasampaida ameshinda Tuzo ya Vijana Wenye Ushawishi Barani Afrika
katika Tuzo zilizotolewa Usiku wa Kuamkia Leo jijini Accra Nchini Ghana Tuzo
Zinazosimamiwa na Uongozi wa Vijana wa Pan African.
Tuzo hizi mashuhuri
zinawatambua Vijana wajasiriamali bora, wanaharakati, waleta mabadiliko na
wafuatiliaji ambao wameonyesha ubora wa kipekee katika nyanja zao Kukiwa na
takriban uteuzi wa vijana 5,000 kutoka nchi 52 za Afrika.
Pongezi za dhati kwa Vijana
100 Wenye Ushawishi Zaidi wa 2025! Mafanikio yako bora yanaendelea kutia moyo
na kuleta mabadiliko katika bara zima na kwingineko.
0 Maoni