Naibu Waziri Mkuu na Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii
pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa ziara ya Mabalozi ya kutembelea vivutio vya
utalii vilivyopo Zanzibar pamoja na
mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Dkt. Biteko amesema hayo leo
Aprili 11, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe.
Kassim Majaliwa katika uzinduzi na ufunguzi wa ziara ya Waheshimiwa Mabalozi ya
katika vivutio vya utalii.
“ Tanzania ni sehemu nzuri
ya utalii duniani na ni imani yangu kuwa mtapata fursa ya kutembelea vivutio
mbalimbali vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa
duniani kwa wapanda milima, lakini pia
tuna hifadhi ya wanyama ya Serengeti, Ngorongoro na sehemu zingine,” amesema
Dkt. Biteko.
Ameongeza “ Mtatembelea pia
Mji Mkongwe Zanzibar na pia mtaweza kujifunza maneno machache ya lugha ya
Kiswahili kupitia ziara hii. Tuna maziwa na mito mingi na maeneo mengine ya
kihistoria kama Bagamoyo na vijiji vya wamasai.”
Pamoja ma hayo, Dkt. Dkt.
Biteko amesema Mabalozi hao wanatakiwa kuendelea kukuza ushirikiano na baada ya
ziara hiyo watakuwa mabalozi wazuri wa utalii wa Tanzania.
Naye, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Balozi Pindi Chana amesema leo ujumbe huo wa Mabalozi utatembelea
vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Ngorongoro, Serengeti na Mlima
Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi amesema baada ya safari
ya Arusha na Zanzibar, mabalozi wataendelea kuitangaza Tanzania kimataifa.
Balozi wa Comoro nchini na
Kiongozi wa Balozi waliopo Tanzania, Mhe. Ahmada El Badaoui Mohammed Fakhi
amesema kuwa kwa takribani miaka 11 aliyokuwepo nchini Tanzania hii ni mara ya
kwanza kwa kuwa na tukio na namna hiyo.
“ Kwa niaba ya Waheshimiwa
Mabalozi wote niipongeze Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje
kwa kuandaa tukio hili,” amesema Mhe. Fakhi.
Na. Ofisi ya Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati
0 Maoni