Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kwamba
hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kusema uchaguzi mkuu usifanyike, hivyo
uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kama ulivyopangwa.
Dkt. Nchimbi
ametoa kauli hizo leo mkoani Songea wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo alikua akigusia kampeni ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya No Reform No Election inayoendeshwa na
Mwenyekiti wake Tundu Lissu.
“Naomba
nizungumzie kidogo kuhusu No Reforms, No Election, tumekuwa tukifanya uchaguzi
mkuu kila baada ya miaka mitano kwa zaidi ya miaka 60, hivyo katika nchi hii
hakuna mtu yeyote, hata rais mwenye mwenye uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike,”
amesema Dkt. Nchimbi.
Amesema pia
ameanza kuona kuna watu wanawalazimisha CHADEMA washiriki uchaguzi mkuu, “Ni
kosa kumlazimisha mtu kushiriki uchaguzi mkuu kwa kuwa ni haki yake kuamua kushiriki
ama kutoshiriki, ila namuomba ndugu yangu Lissu anapogoma kushiriki asiache
haki yake ya kuchagua namuomba kura yake.”
“Kama
wanagomea kuchagua kugomea uchaguzi waacheni ni haki yao msiwalazimishe, hata
hivyo wakina Lissu wanapaswa kujua kama hawajashiriki uchaguzi wa mwaka huu
kuna chaguzi nyingine zitakuja baada ya miaka mitano watakapoamua kushiriki
watashiriki,” amesema Dkt. Nchimbi.


0 Maoni