Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema atahakikisha
katika Ilani ya uchaguzi ya CCM inakuwa na eneo la kuboresha hali ya vyombo vya
habari nchini.
Dkt. Nchimbi
ameyasema hayo leo mkoani Songea wakati akifungua Mkutano Mkuu Maaluma wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo amesema vyombo vya habari ni muhimu
kwa mustakabali wa taifa.
“Tumeshaanza
kuandaa Ilani ya uchaguzi ya CCM na kunamaboresho tunafanya, hivyo basi
nawaahidi kuwa nitahakikisha Ilani ya uchaguzi inakuwa na eneo la kuboresha
hali ya vyombo vya habari nchini,” amesema Dkt. Nchimbi.
Pamoja na
mambo mengine mesema Serikali ya CCM inatambua mchango wa vyombo vya habari
nchini na kuvipongeza vyombo hivyo kwa kuwa makini katika kuhabarisha jamii
jambo ambalo limechangiwa kuwepo kwa amani nchini.
“Amani katika
nchi hii inajengwa na jinsi mnavyoandika habari katika vyombo vyenu vya habari...leo
tunaamani na mshikamano kwa sababu ya kazi kubwa mliyoifanya,” amesema Dkt.
Nchimbi.
Aidha, Dkt.
Nchimbi amewaasa waandishi wa habari nchini kuhakikisha kuwa wakati wa kuelekea
katika uchaguzi mkuu wa 2025 hawatoi habari ambazo zinaweza kuhatarisha amani
ya nchi.
“Mkimkuta mtu
anaongelea masula ya kuhatarisha amani ya nchi ama kuchochea uvunjifu wa amani,
msiandike habari zake, mziache mpite tu kama mmemkuta kichaa akisema maneno ya
hovyo mtaani,” amesema Dkt. Nchimbi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile pamoja na kuipongeza serikali ya Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha uhuru wa vyombo vya habari nchini,
ameiomba serikali kutatua changamoto ya hali mbaya ya uchumi wa vyombo vya
habari nchini.
“Tunaomba
serikali iwe na sera maalum ya kuendeleza vyombo vya habari nchini, jambo hili
sio geni hata katika mataifa mengine linafanyika hilo,” amesema Balile.

0 Maoni