Wajumbe na Watumishi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wapatiwa mafunzo ya e-Mrejesho

 

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Hangi Chang’a akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo wakati akifungua Mafunzo kuhusu Matumizi ya Mfumo wa e- Mrejesho yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Asha Hayeshi akitoa neno la utangulizi kwa baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa Mafunzo kuhusu Matumizi ya Mfumo wa e- Mrejesho yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ndugu Hassan Kilenza akitoa mada kuhusu Mwongozo wa ushughulikiaji wa mrejesho kwa wajumbe wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa mafunzo ya Mwongozo huo yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Utumishi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwadawa Nchemwa akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya Wakuu wa Idara na Vitengo katika Mfumo wa e- Mrejesho kwa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa kikao kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ndugu Hassan Kilenza (hayupo pichani) akitoa mada kuhusu Mwongozo wa ushughulikiaji wa mrejesho wakati wa mafunzo kuhusu Mwongozo huo yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Chapisha Maoni

0 Maoni