Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imeahidi kufanyakazi na Mtandao wa Wana Blogu Tanzania (TBN), pamoja
na vyama vingine vya waandishi wa habari ambavyo vinawakilisha mahitaji na
matakwa ya wanachama wao.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,
Injinia Andrew Kisaka, alipokutana na ujumbe wa TBN ofisini kwake, katika kikao
cha kujadiliana mambo mbalimbali zikiwamo changamoto zinazowakabili bloga nchini.
“Sisi huwa
tunapenda kufanya kazi na vyama ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya
wanachama wao, badala ya kufanyakazi na mwaandishi mmoja mmoja…tunafurahi sana
kufanyakazi na waandishi kupitia vyama vyao,” alisema Injinia Kisaka.
Injinia
Kisaka amesema kuwa TCRA imefurahi kukutana na TBN kwa kuwa wanafahamu kuwa
bloga wanasehemu kubwa sana kwenye maudhui ya ndani, na hata kwenye usajili wa
TCRA bloga wanachukua nafasi kubwa sana katika maudhui ya mtandaoni.
“Kwa hiyo TBN
mtakuwa silaha moja wapo nzuri sana yakutuwezesha sisi kama Mamlaka ya
Mawasiliano nchini, tunao simamia utangazaji pamoja na maudhui ya mtandaoni
kuwa karibu na nyinyi na kuhakikisha maudhui ya mtandaoni yanaleta tija na
maendeleo kwa wananchi,” alisema Injinia Kisaka.
0 Maoni