Tuzidi kumuombea Papa Francis bado hali ya afya yake ni tete

 

Papa Francis amekuwa akipambana na ugonjwa wa nimonia kwa wiki kadhaa, na bado anakabiliwa na shida ya kushindwa kupumua, Vatican imesema.

Hali hiyo imepelekea kuibuka kwa tatizo la kutapika, na kupelekea tatizo la kupumua kuongezeka siku ya Ijumaa, huku akipatwa na kikohozi.

Papa mwenye umri wa miaka 88, imebidi mapafu yake kuingiziwa hewa, kudhibitiwa kutapika na kwa sasa anapata hewa ya oksijeni kupitia kifaa cha kupachikwa usoni ili kumsaidia kupumua.

Vatican imesema madaktari wa Papa Francis wana saa 24 hadi 48 kubaini iwapo amepatwa na madhara ama kudorora zaidi kwa afya yake baada ya kuibuka kwa changamoto hizo mpya.

Chapisha Maoni

0 Maoni