Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Benki ya CRDB wamefanya mazungumzo muhimu kuhusu ushirikiano katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.
Katika mazungumzo yao, TFS na CRDB wameweka mkazo katika kuhakikisha mazingira na rasilimali za misitu zinalindwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Mazungumzo hayo yanayolenga kuimarisha juhudi za uhifadhi nchini yamefanyika jana Makao Makuu ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Ushirikiano huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha Tanzania ya Kijani inawezekana.
0 Maoni