Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imesema kuna uwezekano wa kutokea kiwango cha athari zanazoweza kujitokeza kwenye baadhi ya maeneo ambapo katika baadhi ya makazi yatazungukwa na maji, hivyo basi wananchi wachukue tahadhari.
0 Maoni