Katika kuadhimisha Kilele cha Siku ya Kimataifa ya wanawake
Machi 08, 2025, wanawake shupavu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania - TAWA pia walikuwepo katika mji wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoa
wa Morogoro kuungana na maelfu ya wanawake wengine kutoka mashirika, taasisi
mbalimbali na wanawake wakazi wa Mkoa huo Kwa ujumla wake kuadhimisha siku hiyo
yenye kauli mbiu "Wasichana na Wanawake 2025, Tuimarishe Usawa, Haki na
Uwezeshaji".
Wanawake wahifadhi wa TAWA wamekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha Siku hiyo adhimu katika mikoa mbalimbali nchini na kutumia fursa hiyo kuuonesha umma wa watanzania namna taasisi hiyo inavyotekeleza Kwa vitendo kauli mbiu ya mwaka 2025.
0 Maoni