Wakala ya
Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuwajengea uelewa waandishi
wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu mipango na mikakati ya wakala huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi
Geofrey Mkinga amesema kwamba mkoa wa Dar es salaam katika utekelezaji wa
bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 imeidhinishiwa jumla ya bilioni 68 kwaajili
ya ukarabati na matengenezo ya Barabara Km. 1,151.987 ikiwemo lami Km. 26.04,
madaraja na Kalavati 38.
Amesema
maendeleo ya utekelezaji kwa Mipango ya mwaka 2024/2025 yanahusisha utekelezaji
wa kimaumbile na kifedha ambapo utekelezaji hadi kufikia Disemba 2024 wa kimaumbile
ni asilimia 53.
Kwa upande wa
mradi wa DMDP-II Mhandisi Mkinga amesema jumla ya zabuni 8 za awamu ya kwanza
kati ya hizo, zinajumuisha barabara zenye urefu wa Km. 64 kwa gharama ya
bilioni 190 zilisainiwa Oktoba 23, 2024 na miradi hiyo imeanza rasmi tarehe 15
Januari, 2025.
Ameongeza
kusema kuwa awamu ya pili Zabuni 9 kati ya hizo, zinajumuisha barabara zenye
urefu wa Km. 84.24 kwa gharama ya bilioni 221 zilisainiwa Machi 21, 2025 na
Wakandarasi wanaendelea na kazi za awali za kujenga ‘camp site’ na uwekaji wa
vipimo vya barabara ili kuanza kazi za uondoaji wa miundombinu ya taaasisi
nyingine iliyomo ndani ya eneo la mradi.
0 Maoni