Tanzania ni
nchi ya pili kuwa na kiwango cha chini zaidi cha vitendo vya rushwa kati nchi
kumi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Shirika la Kimataifa la Transparency.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Crispin
Chalamila amebainisha hayo leo Machi 27, 2025 wakati akiwasilisha ripoti ya
utendaji wa taasisi hiyo ya mwaka 2023/2024 kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shirika
Transparency kupitia kiashiria cha CPI ilitoa taarifa hiyo Februari 11, 2025
ambapo kwa mwaka 2024 Tanzania ilipata alama 41 juu ya 100 na kushika nafasi ya
82 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti.
Pamoja na mambo mengine Bw. Chalamila amesema kwa mwaka 2023/24 TAKUKURU ilifanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 30.1 kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa
ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Crispin Chalamila
kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi,
2025.
0 Maoni