Deni la Serikali lafikia Shilingi Tril 97.35 - CAG

 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dkt. Charles Kichere amesema mpaka Juni 30, 2024, deni la serikali lilifikia Sh trilioni 97.35.

Dkt. Kichere ameyasema hayo leo akiwasilisha ripoti yake ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Deni hilo limeongezeka kutoka Sh trilioni 82.25 mwaka wa fedha 2022/2023, ikiwa ni ongezeko la Sh trilioni 15.1 ambalo ni sawa na asilimia 18.36. Kichere amesema deni la ndani ni Sh trilioni 31.95, na deni la nje Sh trilioni 65.40.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023/24 kutoka Bw. Charles Kichere kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Machi, 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni