Wakala ya
Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umesema kwamba utaendelea kujenga
madaraja mengi zaidi kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa mawe kutokana na
ujenzi huo kupunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 80 pamoja na kupunguza
uchafuzi wa mazingira kwa asilimia 75.
Akizungumza katika
semina ya Waandishi wa Habari wa Mitandano wa Jijini Dar es Salaam Mhadisi
Mshauri wa Madaraja ya Mawe wa TARURA,
Pharles Ngeleja, amesema licha ya faida hizo madaraja ya mawe ni imara
na ujenzi wake huwanufaisha wakazi wa eneo husika kwa kupata vibarua.
“Ujenzi wa
madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe umesaidia kupunguza gharama za ujenzi
kwa asilimia 80, ukilinganisha na ujenzi wa madaraja kwa kutumia nondo na zege,
pia unapunguza uchafuzi wa mazingira kwa asilimia 75,” amesema Mhandisi
Ngeleja.
Ameeleza
kwamba tangu waanze kujenga madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe
wameshajenga madaraja 401 nchi nzima, na madaraja hayo yanaweza kudumu kwa
zaidi ya miaka 200 hadi 300 na hayajapata hitilafu yoyote kwa zaidi ya miaka 6.
“Madaraja ya
kutumia teknolojia ya mawe hayajaanza sasa huko Ulaya walijenga madaraja ya
mawe katika miaka ya nyuma hadi pale walipopungukiwa na mawe ndipo wakaacha,
hata hapa nchini madaraja yote ya treni ya TAZARA yamejengwa kwa mawe,” amesema
Mhandisi Ngeleja.
Pamoja na
mambo mengine Mhandisi Ngeleja amesema TARURA pia imekuwa ikijenga barabara za
mawe katika maeneo yanayozunguka makazi, kwa kuwa zinadumu, gharama zake ni
nafuu pamoja kutuharibika zitakapomwagikiwa na mafuta ya magari.
Semina hiyo
iliyowahusisha Jumuiya ya Wanahabari Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA),
ilifunguliwa na Meneja wa TARURA Kingamboni Mhandisi Ismail Mafita kwa niaba ya
Mtendaji Mkuu wa TARURA Victor Seff.
Afisa Habari wa TARURA Bi. Catherine Sungura akitoa maelezo wakati wa semina ya Jumuiya ya Wanahabari Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), ilifunguliwa leo na Meneja wa TARURA Kingamboni Mhandisi Ismail Mafita kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TARURA Victor Seff.
0 Maoni