Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi
ya Nishati endelevu utakaofanyika katika jiji la Bridgetown kuanzia leo tarehe 12
hadi 14 Machi, 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini
humo, Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Mhe. Lisa
Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la
Caribean, Mhe. Humphrey Polepole.
Aidha, Dkt. Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali
kuhusu matumizi ya Nishati endelevu kimataifa ikiwemo Nishati safi ya kupikia
ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya
nishati isiyokuwa safi.
Dkt. Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya
Wanawake, Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar,
Mhe. Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi
Mramba.




0 Maoni