Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Climate
Investment Funds (CIF) Bi. Tariye Gbadegesin Mjini Bridgetown, Barbados.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Machi 14, 2025 kando ya
Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu upatikanaji wa Nishati endelevu kwa wote (Energy
ForAll).
Dkt. Biteko amesema kuwa, Wizara ya Nishati iko tayari
kukuza ushirikiano na Taasisi hiyo ili kuunganisha juhudi za pamoja kuhakikisha
matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan maeneo ya Vijijini.
Aidha, Katika mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mshauri wa Rais Masuala ya Nishati Safi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Angellah Kairuki, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole.



0 Maoni