Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wagonjwa wapatao 6,846 wamepata huduma za
Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni tangu ilipokamilika na kuanza kutoa
huduma.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa
Hospitali hiyo iliyozinduliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake mkoani Tanga.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 7.3
ambapo Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 4.3 na wadau wa Islamic Help
wametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 3.
Amesem mpaka sasa jumla ya majengo yaliyokamilika ni 15
amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga hadi sasa imeshapokea
wajawazito 900 na kati yao 300 walijifungua kwa njia ya upasuaji ndani
ya miaka mitatu(3).
Rais Samia amefanya uzinduzi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara mkoani Tanga ambayo ameanza jana Februari 23, 2025 hadi Machi 1, 2025 kwa lengo la kukagua na kuzindua miradi mbaliambali iliyotolewa fedha na Serikali.
0 Maoni