Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewahakikishi
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano
katika kushughulikia mgogoro wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).
Rais Dkt.
Samia pia ametoa raia kwa Jumuiya hizo mbili kuchukua hatua ili kuhakikisha
kuwa DRC ambayo ni mwanachama wa EAC na SADC, inakuwa salama na mgogoro
unaondelea nchini humo unamalizika.
Rais Dkt.
Samia ameyasema hao leo Februari 8, 2025 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC uliofanyika katika Ikulu ya
Dar es Salaam ili kujadili hali ya usalama Mashariki mwa DRC.
Amesema kuwa
hali inayoshuhudiwa Mashariki mwa DRC haikubaliki na ipo haja ya kuchukua hatua
za haraka kumaliza mgogoro huo unaoleta mateso kwa wananchi."Ninaimani
kuwa mkutano huu utatoka na maazimio ambayo yatawezesha wananchi wa Mashariki
mwa DRC kuishi kwa amani."
Kwa upande
wake Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa EAC, Mhe. William Ruto amesema
mgogoro unaoendelea Mashariki mwa DRC hautomalizwa kwa kutumia silaha bali kwa
njia za kidiplomasia kupitia mazungumzo, kusikilizana na kushauriana.
Aidha, Rais
Ruto amewataka wadau wote kushirikiana na Jumuiya za EAC na SADC katika
kumaliza mgogoro huo ambao unaendelea kugharimu maisha ya wananchi wasio na
hatia.
0 Maoni