Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohammed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa
Ofisi hiyo kuhakikisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Makao
Makuu Dodoma unawasilishwa bungeni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 12 mwaka huu.
Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo jana Februari 6, 2025
katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu la Majengo na
vituo vya daladala jijini Dodoma kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu ya Miji (TACTIC) awamu
ya pili unaotekelezwa chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini
(TARURA).
Amesema Dodoma haiwezi kuwa Makao Makuu kwa matamko pekee,
bali ni lazima kuwe na sheria rasmi itakayohakikisha hadhi yake inalindwa kwa
vizazi vijavyo.
Amesema "Sheria hii iharakishwe kama zinavyoharakishwa
sheria nyingine. Hatuwezi kusubiri tena. Tutamuomba Mheshimiwa Rais kwa hati ya
dharura ili iwasilishwe bungeni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hili."


0 Maoni