Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema ni
marufuku kwa vyama vya upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu
kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.
Wasira ametoa
madaia hayo leo Februari 9, 2025, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya
Nyakonga wilayani Tarime, mkoani Mara.
“CHADEMA wakitaka
kufanya fujo mahali wanakuja kuchukua vijana Tarime.. wawapeleke yaani wao
hawajui kupigana wanaojua kupigana ni wa Tarime, wanakwenda kufanya fujo
wanafanya vijana wa Tarime kuwa majeshi ya kukodisha,” amesema Wasira.
Wasira
amewataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa
wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime
wakiwa na hali mbaya.
0 Maoni