Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje
amedai kuwa sababu iliyomfanya kutofautina na Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Bara, Tundu Lissu pamoja na Godbless Lema ni kukataa kuhusika na mapinduzi ya
mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akiwa gerezani.
Bw. Wenje ameyasema hayo leo Januari 16, 2025 akizungumza na waandishi wa
habari Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tu, tangu Lema azungumze kile
alichodai kuwa Wenje hafai kuwa mwanachama wa Chadema kutokana na sifa zake.
Hata hivyo Wenje ambaye ni mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
wa Chadema Bara, yanakuja ikiwa ni siku chache kuelekea uchaguzi wa chama hicho
huku minyukano baina yao ikiendelea kutoka kwa kambi za wagombe wa nafasi ya
uenyekiti Mbowe na Lissu.
0 Maoni