Watu kumi wamekufa na wengine 30 wamejeruhiwa baada ya
dereva kuendesha gari kwenye kundi kubwa la watu na kuwagonga katika mji wa New
Orleans, nchini Marekani.
Mamlaka za nchi hiyo zimesema katika mtaa wa Bourbon ambao
ni eneo maarufu linalotembelewa na watalii katika mji huo.
Mashuhuda wameviambia vyombo vya habari vya CBS na BBC,
kwamba dereva wa gari hilo baada ya kugonga watu alitoka na kuanza kuvyatua
risasi.
Watu waliojeruhiwa wamepelekwa kwenye hospitali ambapo
timu ya usalama wa umma ipo katika eneo la tukio.
0 Maoni