MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania
Bara, Stephen Wasira amesema Chama na serikali yake haitakubaliana na azimio
lolote litakalotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya
kukutana kwa faragha kama walivyotangaza viongozi wa chama hicho, juzi.
Amesema amesikia chama hicho kikitangaza kwamba kinakwenda
kujifungia kisha kije na jambo ambalo halijapata kushuhudiwa nchini, hivyo
ametoa angalizo jambo hilo ni lazima lifuate sharia za nchi.
Wasira amesema hayo jana alipohutubia wananchi katika
mkutano uliotumika kuzindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa
Chama kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi ya Zamani
mjini Bunda.
“Wamesema wanajifungia halafu waje wafanye jambo ambalo
halijapata kuonekana, nikasema ni jambo gani, mimi nikaona huko kujifungia ile
ni honeymoon maana honeymoon simnaijua, watu wakishaoana wanajifungia
mahali…ile ni honemoon.
“Tunawaambia tunawatakia heri kwenye honeymoon lakini
tunawaambia lolote watakalotoka nalo kwenye honeymoon lazima lifuate sheria,
waklija na honeymoon inavunja amani hatuwezi kuwaunga mkono.
0 Maoni