Zaidi ya watu milioni 10 wameshiriki tendo takatifu la kuoga
kwa ajili ya kujitakasa, katika kusherehekea sherehe ya Wahindu ya Kumbh Mela, ambayo
ni kusanyiko kubwa la binadamu katika mji wa India wa kaskazini wa Prayagraji.
Tukio hilo ambalo hufanyika kila baada ya miaka 12,
limeanza jumatatu na kuendelea kwa wiki sita, ambapo waumini watajitakasa kwa
kuoga kwenye mito inayochukuliwa kuwa ni mitakatifu ya Ganges, Yamuna na mythical
Saraswati.
Wahindu wanaamini kuoga kwenye mito mitakatifu
kunasafisha madhambi, kutakasa roho zao, na kuwakomboa katika mzunguko wa
kuzaliwa na kufa, ili kufikia lengo la kupata ukombozi.
Mahujaji wapatao milioni 400 wanatarajiwa kuhudhuria
sherehe hizo za siku 45, ambazo hupelekea eneo hilo kutokuwa na nafasi kutokana
na umati mkubwa wa mamilioni ya watu wanaofika kujitakasa.
Mamlaka zimesema kwa siku ya Jumatatu watu milioni 10
wamejitakasa kwa kuoga, ambapo kesho jumanne watu watakaokuwa wamejitakasa kwa
kuoga mtoni wanatarajiwa kuzidi milioni 20.
0 Maoni