Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki za Binadamu Mtanzania
Maria Sarungi Tshehai anatarajiwa kuongea leo na vyombo vya habari baada ya
tukio lake la kutekwa jana Jijini Nairobi nchini Kenya.
Maria aliandika katika mtandao wake wa X jana baada ya
kupatikana kuwa, yupo salama kwa sasa na kwamba ataongeza zaidi hapo kesho
(leo).
“Asante sana kesho (leo) nitaongea vizuri, nipo salama,
nimepambana nanyi mmepambana nipo salama asanteni wote Watanzania, Wakenya na
Jumuiya za Kimataifa, kesho (leo) nitaongea .”
Taarifa za kutekwa kwa Maria ziliripotiwa na Shirika la
Kutetea Haki za Binadamu la Amesty International nchini Kenya ambapo lilisema watekaji
hao walifanya tukio hilo majira ya saa tisa na dakika kumi na tano alasiri
wakiwa ni wanaume watatu wenye silaha wakiwa na gari jeusi aina ya Toyota Noah.
0 Maoni