Jeshi la Nigeria limewaua kimakosa raia 16 wa nchi hiyo
katika shambulizi la anga baada ya kudhania kuwa ni kundi la wahalifu.
Wakazi wa eneo lilliloshambuliwa wameviambia vyombo vya
habari walioshambuliwa ni kikundi cha kujilinda na raia wanaojitetea dhidi ya
mashambulizi ya magenge yenye silaha yanayoteka nyara watu na kudai fidia.
Mashambulizi hayo ya anga yalikuwa yanalenga magenge ya
wahalifu katika maeneo ya Zurmi na
Maradun, Gavana wa jimbo hilo Dauda Lawal amesema katika salamu zake za
rambirambi.
Jeshi la Nigeria limekiri kufanya mashambulizi ya anga,
ambayo yamewapa pigo kubwa magenge ya wahalifu wambayo yamemkuwa wakiwataabisha
na kuwatia hofu wanavijiji katika eneo hilo.
0 Maoni